Pages

Friday, July 3, 2015

Habari zenu wanafunzi wangu wa Pre-Course!
Kutokana na maelezo ya mchapaji wetu wa kitabu (Plan B Solutions) kama ambavyo nimekuwa nikiwaeleza darasani, pesa nilizochukua kwenu (Evening Class, Batch A,2&3) hazikutosha kugharamia uchapaji wa kitabu kama tulivyotegemea kwa sababu ya uchache wa pesa yenyewe baada ya kumuomba atupunguzie bei kutoka elfu 10 mpaka elfu 5. Pesa yetu imeshindwa kununua hata "bulk rim" moja ya karatasi za kuchapa kitabu. Kwa kawaida huwa wanachapa kitabu kuanzia nakala 1000 lakini sisi tumetoa pesa watu 116 tu ndo maana alitaka kutuunganisha na wateja wengine ambao kwa sasa hawajawa tayari.Ukubwa wa mzigo wa  mteja mwingine ndio ungenunua hizo karatasi kisha sisi pesa yetu ingegharamia uchapaji na wino tu.Kwa bahati mbaya ndani ya muda huu tunaohitaji kitabu hajapata mteja wa kutubeba.

Niwaombe sana muwe wavumilivu ili pesa hiyo tuiweke akiba kwa ajili ya kitabu cha kozi yenyewe ya Certificate badala ya pre-course kusudi tuendelee kumsubiri mchapaji (printer) apate mtu mwingine wa kutuunganisha ili tubebwe kigharama na watu wengine wanaochapa vitabu vingi.

Kwa sasa nawaomba mjiandae na mtihani kwa kusoma notisi hizi hapa chini na wiki ya tar. 5-10 nitakuja darasani tufanye mazoezi ya kujiandaa na mitihani. Batch A kwa vile siwafundishi someni hizi notisi hapa na kumsikiliza mwalimu Mubarack.Kama kutakuwa na tatizo au hoja tutaongea darasani!

*Notisi zinasomwa kwa ku- "scroll" chini kwenye ukurasa wako wa mtandao.Kama huoni baadhi ya notisi moja kwa moja bofya kwenye "older posts" au "previous posts" au kitu kama hicho kutegemea na "screen" ya kompyuta au simu "smart" uliyonayo!

Nawatakia mafanikio!!!

No comments:

Post a Comment